
Shirikisho
la kandanda barani Afrika CAF limetangaza majina ya wachezaji wa
kiafrika watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2013 na
Mchezaji bora wa Afrika anayechezea vilabu vya ndani ya Afrika mwaka
2013.
Katika
majina hayo yapo majina mawili ya wachezaji wanaotoka Afrika Mashariki
ambao ni Victor Wanyama raia wa Kenya anachezea Southampton FC ya
England
ambaye ni miongoni mwa wachezaji 25 watakaowania tuzo ya
Mchezaji bora wa Afrika, huku Mbwana Samatta raia wa Tanzania
anayechezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
yeye ameteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika anayechezea timu
za Afrika.
Wachezaji 25 watawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika na 21 Mchezaji bora wa Afrika anachezea timu za ndani ya Afrika.
Washindi wa tuzo hizo wanatarajiwa kutangazwa Januari 9, mwaka 2014 mjini Lagos nchini Nigeria.
Orodha kamili ya wachezaji waliotangazwa na CAF na timu wanazotoka hii hapa chini.
Mchezaji wa bora wa CAF Afrika
1. Ahmed Musa - Nigeria - CSKA Moscow
2. Asamoah Gyan - Ghana - Al Ain
3.Dame N'Doye - Senegal - Locomotiv Moscow
4. Didier Drogba - Cote d'Ivoire - Galatasaray
5. Emmanuel Emenike - Nigeria - Fenerbahce
6. Islam Slimani - Algeria - Sporting Lisbon
7. John Mikel Obi - Nigeria - Chelsea
8. Jonathan Pitroipa - Burkina Faso - Stade Rennais
9. Kévin Constant - Guinea - AC Milan
10. Kwadwo Asamoah - Ghana - Juventus
11. Luís Carlos Almada Soares (platini) - Cape Verde - AC Omonia
12. Mehdi Benattia - Morocco - AS Roma
13. Mohamed Aboutrika - Egypt - Al Ahly
14. Mohamed Salah - Egypt - Basel FC
15. Nicolas Nkoulou - Cameroon - Marseille
16. Pierre-Emerick Aubameyang - Gabon - Borussia Dortmund
17. Ryan Isaac Mendes da Graça - Cape Verde - Lille
18. Saladin Said - Ethiopia - Wadi Degla FC
No comments:
Post a Comment