Sunday, 17 November 2013

ANGALIA PICHA YA MWANAMKE ALIYEKATWA MGUU NA MUWE WAKE TARIME

Hali ya wanawake inazidi kuwa mbaya ndani ya nchi yao TANZANIA inayosifiwa kuwa ni Kisiwa cha Amani (Amani kwa wanaume) Tukio hili lilitokea mapema mwezi wa nane mwaka huu Kijiji cha Nyantira Tarime Mara. Katika mazungumzo yake huyu binti alisema kwamba anatamani sana kurudi nyumbani kwa wazazi wake, tatizo ni kwamba kwa kuwa alilipiwa MAHARI na mume wake (aliyemkata panga mguu na kuutoa) hawezi kurudi kwao , wala mama yake hawezi kumkubalia arudi kwao ni mpaka baba yake aje atoe ruhusa ya yeye kurudi nyumbani au abaki kwa mume muuaji avumilie-MFUMO DUME UMEKAMATA MIZIZI (mbayaaaaa, sanaaaa. anajisemeaga Mch Rwakatare)

MBWANA SAMATA KUSHINDANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA



Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF limetangaza majina ya wachezaji wa kiafrika watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2013 na Mchezaji bora wa Afrika anayechezea vilabu vya ndani ya Afrika mwaka 2013.
Katika majina hayo yapo majina mawili ya wachezaji wanaotoka Afrika Mashariki ambao ni Victor Wanyama raia wa Kenya anachezea Southampton FC ya England ambaye ni miongoni mwa wachezaji 25 watakaowania tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika, huku Mbwana Samatta raia wa Tanzania anayechezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo yeye ameteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika anayechezea timu za Afrika.
Wachezaji 25 watawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika na 21 Mchezaji bora wa Afrika anachezea timu za ndani ya Afrika.
Washindi wa tuzo hizo wanatarajiwa kutangazwa Januari 9, mwaka 2014 mjini Lagos nchini Nigeria.
Orodha kamili ya wachezaji waliotangazwa na CAF na timu wanazotoka hii hapa chini.

Mchezaji wa bora wa CAF Afrika

1. Ahmed Musa - Nigeria - CSKA Moscow
2. Asamoah Gyan - Ghana - Al Ain
3.Dame N'Doye - Senegal - Locomotiv Moscow
4. Didier Drogba - Cote d'Ivoire - Galatasaray
5. Emmanuel Emenike - Nigeria - Fenerbahce
6. Islam Slimani - Algeria - Sporting Lisbon
7. John Mikel Obi - Nigeria - Chelsea
8. Jonathan Pitroipa - Burkina Faso - Stade Rennais
9. Kévin Constant - Guinea - AC Milan
10. Kwadwo Asamoah - Ghana - Juventus
11. Luís Carlos Almada Soares (platini) - Cape Verde - AC Omonia
12. Mehdi Benattia - Morocco - AS Roma
13. Mohamed Aboutrika - Egypt - Al Ahly
14. Mohamed Salah - Egypt - Basel FC
15. Nicolas Nkoulou - Cameroon - Marseille
16. Pierre-Emerick Aubameyang - Gabon - Borussia Dortmund
17. Ryan Isaac Mendes da Graça - Cape Verde - Lille
18. Saladin Said - Ethiopia - Wadi Degla FC

Wednesday, 13 November 2013

BARUA YA POLISI WA UINGEREZA KWA TANZANIA KUMTAFUTA GODBLESS LEMA KWA KOSA LA KUMBAKA FLORA LYIMO..!






Hii ni barua ya polisi wa uingereza waliyoandikia polisi ya tanzania wakimtafuta lema akamatwe kwa kosa la ubakaji.

maelezo ya ziada ambayo uingereza walihitaji kutoka polisi ya Tanzania, ni haya hapa chini.

Ushahidi wa mbunge Godbless Lema kumbaka flora lyimo wazidi kubainika

Taarifa za kweli kuhusu mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kumbaka mwanadada Flora Lyimo tarehe 8.8.2012 nchini Uingereza wakati wa ufunguzi wa tawi la chadema nchini humo umezidi kubainika.

Tarehe 2 -3, january 2013 akiwa tanzania, Flora aliwasilisha barua ya polisi wa uingereza kwa polisi kituo cha Moshi mkoani kilimanjaro na kufunguliwa jalada no.MOS/RB/17127/12.

Aidha tarehe 13/12/2012 Afisa upelelezi DC William Hughes wa kitengo cha uhalifu jeshi la polisi la uingereza kituo cha 4-6 shepherdess walk N17LF alifika ubalozi wa Tanzania nchini uingereza ili kujua pamoja na mambo mengine, 
-Taarifa sahihi za GODBLESS LEMA 
-Anuani yake 
-Barua pepe 

Ushauri kutoka mamlaka za Tanzania juu ya mikakati mizuri ya kushughulikia kesi hiyo ambayo inamuhusisha kiongozi wa chama kikubwa cha siasa na 
-Wasifu wake. 

Mbali na tukio hilo kuripotiwa ubalozini, vyanzo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na Gazeti la changamoto la tanzania toleo namba 348 la tarehe 18- 24 desemba 2012 lilichapisha taarifa ya tukio hilo kwenye ukurasa wake wa mbele.kwa kichwa cha habari "POLISI UINGEREZA WAMSAKA LEMA", Pia blog ya global publishers ya nchini tanzania katika report zake za tarehe 14 mei 2013 iliandika habari hiyo kwa kichwa cha habari "MREMBO;MBUNGE AMENIBAKA" Ambapo mrembo huyo (flora) alieleza alivyochaniwa na kufanyiwa kitendo hicho. alieleza kuwa lema alikuwa amemsindikiza mpaka nyumbani na walipofika LEMA aliomba aonyeshwe sehemu ya kujisaidia haja ndogo ndipo alipomvamia Flora na kumchania nguo na kutekeleza azma yake hiyo ovu.

Flora amekuwa akionekana katika shughuli mbalimbali za kijamii lakini ana wasiwasi kuwa anaweza kufanyiwa unyama na LEMA wakati akiwa Tanzania kwa sababu anasema anamfahamu lema pia kuwa ana asili ya ujambazi.

kiambatisho ni barua ya polisi wa kimataifa interpol kumweleza kuwa uchunguzi wa kesi yake unaendelea.

Chanzo:Jamii Forums

"Diamond Platnumz siwezi kumlinganisha hata kidogo na Alikiba..." MASOUD....!SOMA ZAIDI HAPA!

Wiki iliyopita katika kipindi cha Mkasi ambacho hurushwa kupitia EATV na kuendeshwa na mtangazaji Salama Jabir, mgeni alikuwa Masoud Masoud, mtangazaji mahiri wa muda mrefu ambaye ni miongoni mwa watangazaji wa Radio wanaoheshimika sana Tanzania kutokana na upeo mkubwa alionao na kufahamu mambo 
mengi.



Masoud Masoud  
Moja ya swali aliloulizwa ni “Labda kuna tamasha wewe ndio muandaaji au wamekwambia uchague mwanamuziki ambaye ataenda kuburudisha kwenye hilo tamasha Tanzania utamchagua mwanamuziki gani?”

Masoud ambaye anasifa ya kuongea kwa uwazi bila kupindisha maneno alimtaja Alikiba kuwa ndiye msanii pekee wa bongo fleva anayemkubali kuliko mwingine yeyote.

“Mimi wa kwanza nitakayempendekeza aaah nani huyu, nampenda sana katika wasanii wote wa bongo fleva, Alikiba, Alikiba nampenda sana. Alikiba kama umemsikiliza, Rhyme zake zile katikati ya zile bars anavyoimba ni mwanamuziki kama angekuwa nje ya nchi asingekamatika. Angepata producer mzuri wa kumfahamisha nini cha kuimba beat gani atumie, Alikiba yuko juu sana.” Alijibu Masoud

Aliendelea na kuongeza kuwa Diamond anaweza kuwa anafanya vizuri sokoni lakini hawezi kumfikia hata kidogo Kiba katika uimbaji.

“Nyota imeng’aa kwa Diamond Platnumz lakini Diamond Platnumz siwezi kumlinganisha hata kidogo na Alikiba, kwenye kuuza huwezi kumlaumu anaweza kuwa Diamond akauza sana au akampandisha na si Tanzania tu, hata Hollywood wanafanya hivyo hata CBS wanafanya hivyo, hata US music industry wanfanya hivyo. Sasa mpaka wakiwepo watu wataalam wanaoweza kusema huyu anaimba sawa huyu haimbi sawa lakini kwenye mauzo hakuna mtu anajali hilo.”

HAYA NDIO MAISHA...!LADY JAYDEE 'ANACONDA' SASA YUPO MBIONI KUFUNGUA RADIO STATION YAKE.....!!


Nimeshangaa sana baada ya kuona AWARDS mbalimbali alizojinyakulia LADY JAYDEE tokea aanze muziki apa bongo mwaka 2000 hadi sasa 2013,tokea mwaka huo(2000) aanze muziki alibahatika kujinyakulia tunzo na hadi leo hii hajawahi kukosa tunzo ukijumlisha na zile alizopata Uganda kama mara nne au tano.

Hivi,tokea aanze muziki mwaka huo JIDE hajawahi kuchuja hadi leo hii bado yupo juu kimuziki hata kimaisha,kumbuka ni miaka kumi na tatu (13) sasa.Ki ukweli huyu msanii anahitaji heshima ya kipekee apa bongo na nchi za jirani pia.Hiki kitu sio cha kawaida kabisa kuwahi kutokea apa bongo.


Achilia mbali mafanikio aliyoyapata ya kujenga jumba la kifahari,kumiliki mgahawa wa kisasa (NYUMBANI LOUNGE),kumiliki band ya music,kufungua STUDIO YA MUZIKI,na hivi karibuni yupo njiani kufungua RADIO STATION yake binafsi,can u imagine???,kufungua radio station sio kitu cha kawaida hata kidog especially kwa wasanii wetu wa apa bongo.Kwa sasa HAKUNA msanii yeyote awe wa kike au wa kiume mwenye ubavu wa kushindana na huyu bidada,SHE IS THE NUMBER ONE.

Kama ulikuwa hujui huyu ndiyo KOMANDO na huu ndiyo UCHAWI ambao msanii yeyote wa bongo mwingine hajaweza kufanya..!!

PROFESA LIPUMBA AENDA KUIFARIJI FAMILIA YA DR MVUNGI

PROFESA LIPUMBA AKIMPA POLE MKE WA MAREHEMU DR MVUNGI
 


PROFESA LIPUMBA AKISAINI KITABU CHA RAMBI RAMBI

Monday, 11 November 2013

DIAMOND AFUNGUKA JUU YA YEYE KUMUOA WEMA SEPETU...

Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati alifunguka kuwa kwenye maisha yake ya ndoa atakayoingia siku chache zijazo, aliyekuwa mchumba wake wakamwagana na kurejeana hivi karibuni, Wema Sepetu asitegemee kuolewa naye. Diamond ambaye ni staa wa Bongo Fleva aliyasema hayo mbele ya paparazi wetu Novemba 7, mwaka huu jijini Dar kufuatia kuulizwa anamchagua nani wa kumuoa kati ya Wema Sepetu na mchumba wake wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Swali kwa Diamond liliibuka baada ya kuzagaa kwa tetesi kwenye mitandao ya kijamii kwamba yu mbioni kumvisha pete ya uchumba mmoja wa mademu zake.
Swali hilo lilimfanya Diamond afunguke kwa kusema kwamba anachokijua yeye na ambacho kipo kwenye mikakati yake, mke wake mtarajiwa ni Penny. “Najua wengi wanahisi mimi ninaweza kuoa mwanamke zaidi ya mmoja kutokana na dini yangu kuruhusu lakini jambo hilo mimi silifikirii hata kidogo kwa kuwa kwenye maisha yangu nilishapanga nitaoa mke mmoja tu,” alisema Diamond. Akaendelea: “Watu wanasema mengi juu yangu na Wema, wengi wao hawajui nafsi yangu inataka mwanamke yupi, ninachoweza kusema na watu wakasikia na kunielewa basi wajue kwamba Penny ndiye mke wangu, Wema asitegemee kuolewa na mimi.” Diamond alikwenda mbele zaidi kwa kumwanika Penny kwamba ana sifa ya kuwa mke kwani ni mvumilivu sana na anaonesha upendo wa dhati kwake. “Kwa maana hii basi hakuna mwanamke mwenye jina  kubwa wala sura nzuri zaidi ya Penny ninayeweza kumwita mke wangu. Najua kila mtu ana namna yake ya kuchagua ampendaye, ndiyo maana utaona watu wanasema hili mara lile, lakini hawajui nafsi yangu inataka mwanamke wa aina gani,” alisema Diamond na kuongeza: Kama kuna demu anayejipa matumaini hayo basi asitegemee hata siku moja kwa sababu kuoa kwangu kutazingatia mke mwema na si bora mke, Penny pekee ndiye mwenye sifa za kuwa mke wangu,” alisema Diamond. Juzi Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Penny ili kutaka kupata maoni yake kuhusu tamko la Diamond, lakini muda mrefu simu hiyo ilikuwa ikiita bila kupokelewa. Baada ya kumkosa Penny, Ijumaa Wikienda lilimtwangia simu Wema, naye kama Penny, simu yake iliita mara kadhaa lakini haikupokelewa
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget

Saturday, 9 November 2013

HATIMAYE MAMA DIAMOND AZUNGUMZIA PENZI JIPYA LA WEMA SEPETU KWA DIAMOND, UNAJUA KASEMA NINI? SOMA HAPA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg6LFcmL5SHgtI1IChyphenhyphenN6NPO0ki72N3qkZHUOZWVMCUCN4I7vl5TAJfJ_-eadOXZ5SbftJNbBDbZhkXN7ca8seHUwh4WbwvoPSjXwvUOL8fGzlzsFIFbQga1I6Yrai20l2AMXH50CHXSfY/s640/4.jpegMsanii wa ngoma ya Number One, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameingilia kati penzi lililofufuka upya kati ya mwanaye na staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu.
Habari za chini ya kapeti zilitonya kuwa baada ya kuambiwa na kuoneshwa picha za Diamond akiwa kimahaba na Wema alikuja juu akidai kuwa hamtaki Wema kwa kuwa anamkubali zaidi Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Akizungumza akiwa  nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar wikiendi iliyopita, bi’mkubwa huyo alisema kuwa kwa sasa hafahamu chochote kuhusu Diamond kurudiana na Wema zaidi ya kusikia kwa watu na kuona picha katika mitandao ya kijamii.
“Kuhusu Nasibu (Diamond) kurudiana na Wema, nasikia tu na kuoneshwa picha namsubiri Nasibu arudi kisha nikae naye ndipo nitatoa tamko,” alisema mzazi huyo.
Mapaparazi wa Ijumaa Wikienda kadiri walivyozidi kumchimba mama mkwe huyo wa Wema ni jinsi gani anavyojisikia kuhusu tabia ya kubadilisha wanawake kama nguo, ikizingatiwa yeye ni mzazi haoni kama mwanaye anamfedhehesha alisema kuwa hayo ni maisha yake.
“Hayo ni maisha yake na mwenyewe kwa kuwa ameshazoea kuonekana katika magazeti kila wakati mi niongee nini wakati ndiyo maisha aliyojiwekea,” alimalizia kusema.

HUYU NDIYE MCHAWI ALIYEDONDOSHWA NA MAOMBI YA MAKOMANDOO WA VHM ALFAJIRI

Makomandoo wa VHM wakiwa katika Operation ya kusambaratisha kazi za shetani afajiri baada ya maombi mazito mama aliyekuwa na tumbo kubwa akidhaniwa ni mjamzito kumbe hakuwa na mimba yoyote. Baada ya maombi mazito chini ya usimamizi wa makomandoo ya Yesu kupitia Voice of Hope Ministry  alijikuta akitapika meno ya mbwa, nywele na vitu visivyojulikana. Siku chache

WATACHOMOKA KWELI

WAUAJI WA UNITED KESHO

Mesut Ozil

TEAM NEWS: WHO IS FIT


Matchday Show - Manchester United v Arsenal

ARSENAL:Normally, Flamini and Walcott will join us in the session this morning. Wilshere will join in as well, so we will see how they are after the session today. 

UNITED: David Moyes will be hoping to have Michael Carrick, Jonny Evans and Rafael in contention after injuries ruled the trio out of the trip to San Sebastian. Marouane Fellaini will be available as the suspension for his red card at Estadio Anoeta, of course, only applies in Europe. Jack Wilshere was due for tests on the injured ankle that sidelined him for the Liverpool and Dortmund fixtures, but Arsene Wenger was more hopeful over the possibility of a return for Theo Walcott and Mathieu Flamini.

(Official Music Video) Nay wa Mitego ft. Neiba - Salam Zao

ANGALIA PICHA JUMA KASEJA AKISAINI MKATABA YANGA

 















Mlinda mlango nambari moja nchini Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka 10 mfululizo Juma Kaseja Juma jana majira ya saa 2 usiku alisaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Young Africans yenye makao yake Twiga/Jangwani kwa kipindi cha miaka miwili.
Usajili wa Juma Kaseja kujiunga na klabu ya Yanga unafuatia mapendekezo ya benchi la ufundi katika ripoti waliyoikabidhi kwa kamati ya mashindano kwa ajili ya kuboresha kikosi






Juma Kaseja akisani mkataba wa kuicheza Yanga kwa miaka miwili mbele ya mwenyekiti wa kamati ya mashindano Bin Klebl


KASEJA APATA ZALI

Kipa Juma Kaseja amesaini mkataba wa kuichezea Yanga rasmi, mkataba huo umesainiwa jana Ijumaa na ataanza kuitumikia timu hiyo katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Kaseja amesaini kwa dau la Sh milioni 40.

NIPO TAYARI KUCHANGIA PENZI LA DIAMOND PLATINUMZ NA WEMA SEPETU: VJ PENNY

Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha DTV, Peniela Mwingilwa ‘Penny’, ambaye ni mpenzi wa mkali wa Bongo Fleva Diamond Platinumz amesema yupo tayari kuchangia mapenzi na msichana mwingine yeyote ambaye atachukuliwa na mwanaume huyo anayempenda.

Penny katika Penny na Wema.

Penny ambaye ni chaguo la mama mzazi wa staa huyo wa kibao cha My Number One, aliiambia Globalpublishers  maneno hayo, yanayotafsiriwa kama yupo tayari kuchangia mapenzi na hasimu wake, Wema Sepetu ambaye ni Miss Tanzania 2006n na muigizaji wa filamu Swahiliwood

Friday, 8 November 2013

MAITI YAKUTWA NA KETE 600 ZA DAWA ZA KULEVYA


 Kete inayosadikika kumuua kijana huyo baada ya kupasukia tumboni.

WANAFUNZI WAWILI WA CBE WAPATA AJALI YA PIKIPIKI NA KUFARIKI MKOANI DODOMA


 Baadhi ya watu wakiisogeza miili ya Wanafunzi wa CBE Dodoma  walikufa kutokana na kuligonga tela la lori kwa nyuma kutokana na mwendo kasi huku lori hilo likiwa limetelekezwa zaidi ya wiki bila alama yoyote barabarani hapo.
Miili ya Marehemu Ramadhan Lesso na Gerge Lwandala inaonakana kabla ya kuondolewa katika kijiji cha Ihumwa barabara ya Morogoro Dodoma kabala ya kuondolewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospital ya mkoa.

MTOTO AWA NA MIGUU MISITA