Wednesday, 24 April 2013

AVRIL KUACHIA SINGLE YAKE MPYA NA OMMY PIMPOZ TAR 30 APR

MSANII WA BONGO FLEVA 2NDA MAN KATIKA MUONEKANO MPYA WA NYWELE

Msanii kutoka kundi la Tip Top Connection maarufu kama Tunda Man ameonekana kubadili muonekano wake wa zamani na sasa kuja na mpya ....
Muonekano huo mpya wa style ya nywele zake [pichani] umeonekana kuwashangaza watu kwa jinsi ulivyokuwa wa kipekee ...
Haijafahamika ameutoa wapi na ni kwa ajili gani anautumia, ila hivi ndivyo anavyoonekana sasa Tunda Man kichwani kwake .

Saturday, 20 April 2013

UNAMJUA HUYU

MSIMAMO LIGI KUU ENGLAND


Position Team Played Goal Difference Points
1 Man Utd 33 40 81
2 Man City 32 31 68
 3 Arsenal 34 30 63
 4 Chelsea 32 31 61
 5 Tottenham 32 15 58
 6 Everton 34 13 56
7 Liverpool 33 19 50
8 West Brom 33 -1 45
 9 Swansea 33 1 42
10 West Ham 34 -7 42
 11 Fulham 34 -8 40
 12 Southampton 34 -7 39
 13 Norwich 34 -20 38
14 Sunderland 34 -7 37
15 Stoke 34 -11 37
16 Newcastle 34 -17 37
 17 Aston Villa 33 -24 34
 18 Wigan 33 -23 31
 19 QPR 34 -27 24
 20 Reading 34 -28 24

ARSENAL YAICHAPA FULHAM



Per Mertesacker (second right) celebrates his goalHatimaye klabu ya ligi kuu ya England washika bunduki wa jiji la london wamefanikiw kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya clab ya fulham,bao la arsenal lilifugwa mnamo dakika ya 43 kupitia beki wake mahili wa timu ya taifa ya ujerumani per mertesacker kufuatia kuunanisha vizuri klosi iliyotua kichwani mwa beki koscielny na per kumalizia.

SEREKARI YA TANZANIA YATANGAZA KUHUSU DARASA LA SABA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU



 


http://www.mwananchi.co.tz wameripoti leo kwamba Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao ambapo udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.
Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B ambapo Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia Mwananchi kwamba baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.
Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine, Sifa zinazotakiwa ili kujiunga…. mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba,  atakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma, awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuo

JE WAMJUA HUYU

Chinua Achebe (Associated Press/Craig Ruttle)