Saturday, 22 June 2013
BOB JUNIOR APEWA KIPIGO KIKALI KARIAKOO BAADA YA KUIBA....NI KATIKA UTENGENEZAJI WA VIDEO YAKE MPYA YA KIMBIJI
Friday, 21 June 2013
WANAFUNZI UDSM WAPIGWA RISASI

Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao na pochi za fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha, na majambazi kuanza safari yao.
Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.
Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa hakuna majibu na ndipo walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi. Kwa sasa mwanafunzi huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka, ingawa FULLSHANGWE inajitahidi kufuatilia suala hilo ili kupta taarifa zaidi na picha za tukio hilo.
HOUSEGIRL AJIRUSHA KUTOKA GHOROFANI

Tukio hilo lilijiri mapema asubuhi ya Juni 18, mwaka huu kwenye makutano ya Mtaa wa Nyamwezi na Mkunguni eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa majirani, baada ya kuona moto huo ulioambatana na wingu zito la moshi ukitoka kwenye jengo la jirani, hausigeli huyo alitoka dirishani na kutaka kujirusha chini bila kujali nguo zilizokuwa zikimvuka katika purukushani hiyo.
Alifanikiwa kukaa kwenye sehemu ya ukingo wa ghorofa hilo na kujiandaa kwa tukio la kwenda chini akiamini atakuwa amejiokoa na moto huo.
Hata hivyo, bosi wa hausigeli huyo alipoona zoezi hilo la hatari alitoa mkono dirishani na kumvutia ndani mfanyakazi wake huyo tukio ambalo lilijiri muda mfupi kabla ya Kikosi cha Zima Moto kufika na kufanikiwa kuuzima bila kujeruhi mtu.
NAY WA MANZESE AMPIGISHA MLEGE DEMU WAKE
![[clip_image002%255B5%255D.jpg]](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-398pKF0_KZkq0Xjmc6OoxzYZFy9fKQStJzqJZlqPksfT-vaXeA-nabbKit7KDnNeg3_4kA5h28dmP9Otu0BKfJW4CdKgSERNEFgMNFLwhbJrTGmu8sn3FRBS11Rslkk54qqsnrsh9gw/s1600/clip_image002%25255B5%25255D.jpg)
Thursday, 20 June 2013
DEMU WA BALLOTELI AWA KIVUTIO UWANJANI BRAZIL

uwanjani wakati Italia inacheza na Japan huku akiwa amevalia jezi ya Italia.
Kwa wasiomfahamu wanaweza kudhania kuwa mwanamitindo huyo ni raia wa Italia kwa uzalendo aliouonyesha akiwa uwanjani lakini yeye ni raia wa Ubelgiji . Uwepo wa Fanny uwanjani unaonekana kumsaidia Super Mario ambaye alifunga moja ya mabao yaliyoisaidia Italia kushinda 4-3.
Hivi karibuni Mrio alimvika mpenzi wake Fanny pete ya uchumba yenye thamani ya paundi laki moja baada ya tetesi kuwa zimesikika juu ya wawili hao kuachana kwenye mataa.
Tuesday, 18 June 2013
SABABU ZA JESHI LA POLISI KUTUMIA NGUVU YA MABOMU JIJINI ARUSHA MUDA HUU

Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo .
Akizungumza
ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema
kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo
imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu
upelelezi.
Kamanda Sabas amedai kuwa jeshi la polisi liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.
Hali
kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi
wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya
kuomboleza ..
Wakati mabishano hayo yakiendelea, Askari Polisi mmoja alijichanganya na kuingia
katikati ya wafuasi wa Chadema pembeni mwa uwanja huo ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu
wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa na bomu June 15 2013.
BreakingNewzzzz...:Sugu apata ajali akiwa njiani kuelekea Arusha
..Mbunge
wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi amepata ajali hivi punde katika eneo la
kasheki wilayani Hanan'g akielekea Arusha mjini.
Joseph Mbilinyi maaru Sugu alikuwa
akielekea Arusha mjini kuungana na wabunge wengine ktk shughuli ya kuaga
marehemu
waliolipukiwa na bomu kwenye mkutano wa Chadema, mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Katika ajali hiyo hakuna mtu yoyote
amejeruhiwa, Mbunge huyo yuko salama, gari la Sugu limeharibiwa vibaya
baada ya kugongana na basi la abiria.

MTANZANIA NANDO HATARINI KUTOLEWA BIG BROTHER ..KURA YAKO MUHIMU KUMUOKOA
Ni wiki tatu zimepita tukishuhudia Eviction shows tatu zilizowapa
tiketi za kurudi makwao washiriki 6 mpaka sasa, na tumeshuhudia mshiriki
wetu Feza Kessy akiponea kwenye tundu la sindano baada ya kura za wa
Tanzania na wa Afrika kumuokoa, sasa ni zamu ya Nando ambaye yuko
hatarini wiki hii.
Big Brother jana ametaja majina ya washiriki 7 ambao wako hatarini
kutoka wiki hii na kati yao yupo kijana mpole, mtanashati, ‘handsome’
Nando anaeiwakilisha Tanzania, ikiwa ndio mara yake ya kwanza
kupendekezwa .
Washiriki wengine walipigiwa kura nyingi kutoka wiki hii ni love
birds Bolt na Betty, ambao hii si mara yao ya kwanza kupendekezwa baada
ya kuponea chupuchupu kwa mara kadhaa.
Kenya wiki hii iko salama kwa mshiriki wao mmoja aliyesalia Annabel,
japo kuwa alipendekezwa kutoka wiki hii lakini kilichomuokoa ni yeye
kuwa mkuu wa nyumba ya Diamond, hivyo amepata favor ya kujiokoa
mwenyewe na nafasi yake akampendekeza Motamma wa Botswana.
Kwa ujumla walioingia wiki hii ni Nando wa Tanzania, Natasha wa
Malawi, Oneal wa Botswana, Motamma wa Botswana, Betty wa Ethiopia, Bolt
wa Sierra Leon na Elikem wa Ghana.
Tanzania bado ina nafasi nzuri sababu washiriki wote wawili Nando na
Feza wapo mjengoni na ndio maana unakila sababu ya kumpigia kura mara
nyingi uwezavyo Nando ili aweze kubaki wiki hii.
Washiriki wawili kati
ya saba waliopendekezwa watapita kwenye mlango wa ‘EXIT’ mjengoni hapo
Jumapili hii (June 23) wakati wa Eviction Show.
Monday, 17 June 2013
SINTAH AMTOLEA UVIVU OMMY DIMPOZ NA KUMPA LAKE LA ROHONI

Sinta ameandika haya yafuatayo katika website yake:
MDOMO UMEMPONZA HUYU KIJANA
sasa wewe unataka kuniambia u have invested na hutegemei show?? kumbuka sisi mashabiki wako ndio tumekuweka hapo juu na ku support music wako haya tukiacha kupenda nyimbo zako na ukakosa show itakuwaje??? umenizije sasa kumkejeli mwenzio tena kwenye kipaza sauti next time uliza nini cha kuongea ndio maana wenzenu wanakuwa na managers wa kuwa guide sio unaongea tu coz usikike. wenzio walionyamaza uliwaona mafala sio?? au ulitaka utoke kama hivi tukuongeleee cheap cheap fame.
kauli yako uko sahihi ila kwanini usingeiongelea ktk interviews zako kama ushauri kwa wasanii wenzio na ukaifanya ni big issue ktk msiba wa mwenzio??
nimekupa langu la roho kazi kwako sasa ukinichukia sijali, ukinipenda sawa coz naongea ukweli na wananchi waliokerwa wamenituma na sikuwepo ila wamerekodi wakaniambia CEO ifanyie kazi Ommy D katukwaza" says Sintah
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
ASANTE KWA KUPATA HUDUMA ZETU,TUNAKUOMBA BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK
Subscribe to: Post Comments (Atom)
page counter
?
X
Recommended for you
STEVEN KANUMBA JR AZALIWA, MAMA KANUMBA, MAMA LULU NA LULU WAJAWA NA FURAHA.

PICHA YA MTOTO ALIYEZALIWA AKIWA NA MIGUU SITA

Huyu ni binadamu mwenzetu aliyezaliwa akiwa na miguu sita.Anakaaje, anasimama vipi.....na anatembeaje.....Yote tumwachie mungu aliyeamua iwe hivyo
Subscribe to:
Posts (Atom)
No comments:
Post a Comment