Friday, 31 May 2013

DIAMOND AENDELEA KUWEKA WAZI MAISHA YAKE YA KIMAPENZI, HIKI NDO ALICHOKISEMA. SOMA HAPA

Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameibuka na kuelezea kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye ni mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali Tanzania

Akizungumza kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi Jokate kwa sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila yeye ndiye tatizo na chanzo cha kuachana
kwao.
DIAMOND ANAFAFANUA

“Inanipasa nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa mapenzi yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote kinyume. Sijui niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo sababu ya kuachana kwetu na ilitokea tu.

“Naamini hilo jambo lilimuuma sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya mimi kurudi kwa Wema (Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo hivyo, siwezi kufafanua zaidi.

“Kutoka moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama hatanisamehe nitaendelea kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha kabisa kutokana na jambo hilo. Lazima niwe mkweli.”

No comments:

Post a Comment