Friday, 31 May 2013
MTANZANIA FEZA AZIDI KUNGA'ARA BIG BROTHER AFRICA....AUKWAA UKUU WA KAYA

Tunaenda vizuri, bahati inaonekana kutuangukia watanzania kwani
mshiriki Feza jana ameukwaa ukuu wa kaya ama kwa lugha ya ki-big brother
‘Head of House’.
Ilikuwaje?
Baba mwenye nyumba, biggie, alitoa task ambayo washiriki walitakiwa
kuelekea bustanini na kuchagua box, ambaye angechukua box la ushindi ndo
huyo angekuwa mkuu wa kaya. Kama zali, bahati hiyo ilimuangika mrembo
Feza. Washiriki wenzie akiwemo mtanzania Nando, walimkumbatia kwa furaha
kama ishara ya kumpongeza.
Iko hivi, ukichaguliwa kuwa mkuu
wa kaya, unauwezo wa kumuokoa mtu ambaye anakuwa amependekezwa atoke
katika wiki hiyo. Usipofanya hivyo basi wewe mwenyewe unawekwa
kikaangoni.
Feza alitumia nafasi hiyo kumuokoa Elikem ambaye
ni mshiriki kutoka Ghana na kumuweka kikaangoni Betty kutoka Ethiopia.
Hiyo ni siri ambayo Feza inabidi aitunze hadi siku ya Jumapili wakati wa
Eviction.
Hii issue ya kumuokoa Elikem wa Ghana, je ni dalili ya shemeji shemeji mbona wazima taa? Endelea kufuatilia..
HII NDIO SABABU INAYODAIWA KUSABABISHA KIFO CHA NGWAIR. SOMA HAPA

Africa Kutoka Kwa Hussein
Original Ambaye Yupo Pretoria
Amesema Ngwear Amefariki Leo
Asubuhi. Alikuwa Ghetto Moja Na
Msanii M To The P.
Walivyokwenda Kuwagongea
Asubuhi Walikuta Ngwear
Amefariki Na M To The P
Amepoteza Fahamu Kabisa. Pia
Daktari Ameshatoa Taarifa Kwa
Watu Wa Karibu Wa Ngwear
Huko South Africa. Ngwea akiwa na msanii M to the P jana south africa.mtu wa karibu anasema walitakiwa kurudi dar leo lakini waliwakuta wamezima kwenye room wote wawili baada ya kuji overdose madawa ya kulevya na M to the P yupo hoi hospitali
DIAMOND AENDELEA KUWEKA WAZI MAISHA YAKE YA KIMAPENZI, HIKI NDO ALICHOKISEMA. SOMA HAPA

Akizungumza kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi
Jokate kwa sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila yeye
ndiye tatizo na chanzo cha kuachana
kwao.
kwao.
DIAMOND ANAFAFANUA
“Inanipasa nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa mapenzi yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote kinyume. Sijui niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo sababu ya kuachana kwetu na ilitokea tu.
“Naamini hilo jambo lilimuuma sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya mimi kurudi kwa Wema (Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo hivyo, siwezi kufafanua zaidi.
“Kutoka moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama hatanisamehe nitaendelea kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha kabisa kutokana na jambo hilo. Lazima niwe mkweli.”
Tuesday, 21 May 2013
Tuesday, 14 May 2013
Sunday, 12 May 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)